Ninafaa kujua nini kuhusu diaphragm

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ninafaa_kujua_nini_kuhusu_diaphragm

Diaphragm ni mpira ulio kama kikombe uliotengenezwa na mpira laini au silicone nyembamba ambayo mwanamke huvaa katika uke wake wakati wa kujamiiana. Diaphragm hufunika mlango wa uzazi ili shahawa ya mwanamume isiingie katika tumbo la uzazi.

Wakati diaphragm inapotumika vyema au kwa usahihi, kwa wakati mwingi huzuia mimba na pia huweza kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Diaphragm lazima itumike kwa spermicide. Ikiwa huna spermicide, bado unaweza kutumia diaphragm, lakini inaweza kosa kufanya kazi vyema ili kuzuia mimba.

Diaphragms huja katika saizi tofauti, na hupatikana katika baadhi ya vituo vya afya na kliniki zinazotoa huduma za upangaji uzazi. Mhudumu wa afya aliyefunzwa kufanya uchunguzi wa sehemu ya pelvic anaweza kukuchunguza na kupata saizi ya diaphragm inayokufaa. Diaphragm hufanya kazi vyema bora tu utumie saizi inayokufaa.

Diaphragm yaweza kupata mashimo, haswa baada ya kutumika kwa zaidi ya mwaka. Ni vyema kuangalia diaphragm yako mara kwa mara. Badilisha wakati diaphragm itakuwa kavu au ngumu, au wakati kuna shimo ndani yake.

Unaweza kuweka diaphragm ndani kabla tu ya kujamiiana au hadi masaa 6 kabla ya kujamiiana. Ikiwa utashiriki ngono zaidi ya mara moja baada ya kuweka diaphragm ndani, weka spermicide zaidi ndani ya uke wako kila wakati kabla ya kujamiiana, bila kuondoa diaphragm.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020414