Ninafaa kujua nini kuhusu mzunguko wa vurugu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ninafaa_kujua_nini_kuhusu_mzunguko_wa_vurugu

Shambulizi la kwanza mara nyingi huonekana kama tukio la kipekee. Lakini katika visa vingi, baada ya ghasia hutokea kwanza mifano ifuatayo, au mzunguko, huendelea:

Vurugu hutokea: kupiga, kuchapa kofi, kupiga mateke, kusakamwa, matumizi ya vitu au silaha, unyanyasaji wa kijinsia, vitisho vya matusi na unyanyasaji.

Kipindi cha utulivu hufuatia vurugu: Mwanamume anaweza kukataa/kukana vurugu, kuomba msamaha au kuahidi kwamba kamwe haitatokea tena.

Kisha polepole mvutano unaanza tena: hasira, majibizano, kulaumiana, matusi.

Vurugu inatokea tena. . . .

Wakati vurugu inapoendelea, kipindi cha utulivu huwa kifupi na kifupi kwa wapenzi wengi. Huku nia ya mwanamke huvunjwa, mamlaka ya mwanamume kwa mwanamke yanaongezeka hadi inakuwa si lazima kwake kuahidi kuwa mambo yatakuwa sawa.

Baadhi ya wanawake hujaribu kusababisha vurugu ndiposa iishe haraka, ili kurudia kipindi cha utulivu haraka.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020110