Ninaweza kufanya nini kwa ajili ya usalama wangu wakati nitakapo kuwa tayari kuondoka

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ninaweza_kufanya_nini_kwa_ajili_ya_usalama_wangu_wakati_nitakapo_kuwa_tayari_kuondoka

Hifadhi pesa/fedha kwa njia yoyote ile utakayoweza. Weka pesa mahali salama (mbali na nyumba) au fungua akaunti ya benki ukitumuia jina lako mwenyewe ili uweze kuwa huru zaidi.

Ikiwa unaweza kufanya hivyo kwa usalama, fikiria mambo mengine unayoweza kuyafanya ili usimtegemee sana, kama vile kuwa na marafiki, kujiunga na kikundi, au kujumuika na familia yako kwa muda mrefu.

Je, una ujuzi unaoweza kuutumia ili kupata pesa/fedha za ziada? 

Angalia ikiwa kuna 'nyumba zilizo salama' au huduma nyingine za wanawake ambao wamekuwa wakidhulumiwa vibaya. Hizi ni sehemu maalum katika baadhi ya miji na majiji ambapo wanawake waliodhulumiwa na watoto wao wanaweza kukaa kwa muda. Jaribu kujua kabla ya kuondoka ikiwa kuna moja ya hizo unaweza kupata.

Waulize marafiki au ndugu unaowaamini ikiwa wanaweza kukubali ukae nao au kukukopesha pesa. Hakikisha kwamba hawatamwambia mpenzi wako kwamba ulipata msaada kutoka kwao.

Pata nakala za nyaraka muhimu, kama vile kitambulisho chako au kumbukumbu za chanjo ya watoto wako. Weka nakala nyumbani na upeane nakala nyingine kwa mtu unayemwamini. Wacha pesa/fedha, nakala ya hati yako, na nguo za ziada na mtu unayemwamini ili uweze kuondoka haraka.

Ikiwa unaweza kufanya hivyo kwa usalama, fanya mazoezi ya kutoroka kwako na watoto wako ili kuona kama utafaulu. Hakikisha kwamba watoto hawatamwambia mtu yeyote.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020118