Ninawezaje kujitetea mwenyewe

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ninawezaje_kujitetea_mwenyewe

Fanya mazoezi haya ya ulinzi ya kujitetea ukiwa na rafiki yako, ndiposa uwe tayari kupigana na mshambulizi.

Mpige kwa nguvu unavyoweza. Usioogope kumuumiza- kwani yeye haogopi kukuumiza.

Ikiwa utashambuliwa kutoka nyuma.

  • Mgonge ukitumia nguvu kwa tumbo lake ukitumia elbow yako.
  • Mkanyage mguu wake ukitumia kisigino chako cha mguu.
  • Tumia mkono wako, kushika korodani zake (mipira), kisha zifinye kwa nguvu.
  • Ukitumia kisigino chako, mpige teke kwa nguvu chini ya mguu wake au goti.

Ikiwa utashambuliwa kutoka mbele

  • Ukitumia vidole vyako mdunge macho yake.
  • Tengeneza ngumi kwa mikono yako miwili na umgonge sehemu zote mbili za upande wa kichwa chake, au juu ya masikio yake.
  • Tengeneza ngumi kisha umgonge ukitumia nguvu juu ya pua lake.
  • Inua magoti, na usukume kwa haraka kama unaweza katika korodani zake (mipira).

Njia zingine za kujitetea ni:

  • Ikiwa uko katika eneo la umma kisha mtu ajaribu kukuumiza au kukunyanyasa, piga kelele kwa sauti kubwa uwezavyo.
  • Fanya jambo litakalomkera kama vile kutema tema mate, au jifanye unatapika, au fanya jambo la kiuwendawazimu.
  • Ikiwa anayekunyanyasa ni jamaa wa famili yako, jaribu kuzungumza kuhusu suala hilo na jamaa mwingine wa familia unayemwamini.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020311