Ninawezaje kumzuia mtoto wangu kutokana na majeraha ya nyumbani

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ninawezaje_kumzuia_mtoto_wangu_kutokana_na_majeraha_ya_nyumbani

Glasi iliyovunjika yaweza kusababisha kujikata, upungufu wa damu na vidonda. Vyuma vilivyonolewa, mashine na makopo yaliyo na kutu yanaweza kusababisha vidonda vinavyoweza kusababisha maambukizi.

Familia zinaweza kupunguza hatari za kuumia kwa mtoto kutokana na gilasi na vifaa vilivyonolewa ikiwa;-

Wataweka chupa za gilasi mahali mtoto hataweza kuzipata na kuweka nyumba na mahali pa kuchezea pasafi bila gilasi zilizopasuka na kukataa

Kuweka visu, nyembe na makasi katika drawers au kabati zilizofungwa ambazo watoto hawawezi kuzifikia.

Tupa takataka vyema, ikiwemo chupa zilizovunjika na makopo yaliyozeeka.

Waweza kuzuia majeraha nyumbani kwa kuwafunza watoto wako kuhusu hatari za kutupa mawe au vifaa vilivyonolewa na kucheza na visu au makasi.

Mifuko ya plastiki yapaswa kuwekwa mbali na watoto ili kuzuia wao kupata ukosefu wa hewa.


Sources