Ninawezaje kupata huduma za kuavyaa mimba zizlizo salama

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ninawezaje_kupata_huduma_za_kuavyaa_mimba_zizlizo_salama

Wakati mwanamke anapopata mimba asiyoitaka anastahili kupata huduma bora za kuavyaa mimba na zilizokubalika kisheria. Lakini, sheria za utoaji mimba ni tofauti kwa kila nchi.

Uavyaji mimba uliokubalika kisheria: ikiwa kuavyaa mimba ni halali, mwanamke anaweza kwenda katika huduma za kiafya au hosipitalini, kisha alipe, halafu atolewe mimba salama. Katika nchi ambapo haya hutokea sio wengi hugonjeka au kufa kutokana na matatizo ya kuavyaa mimba.

Kuavyaa mimba kuliko kubaliwa kisheria kwa wakati mwingine: Katika nchi zingine utoaji mimba umekubaliwa kutokana na sababu chache ambazo ni:-

  • Ikiwa mwanamke atakuwa mjamzito baada ya kubakwa au kushiriki ngono na mtu wa familia.
  • Ikiwa daktari atasema kuwa mimba hiyo ni hatari kwa afya ya mama.

Lakini kuavyaa mimba huwa ni vigumu hata kama ni kwa sababu ya hizo sababu. Madaktari na wahudumu wa afya huenda wakakosa kuelewa nini haswa sheria inavyosema. Wanaweza kukataa kufanya shughuli hiyo au wanaweza kuitisha pesa nyingi. Wanawake wanaweza kosa kujua ikiwa kuavyaa mimba kumeidhinishwa katika nchi yao au la.

Ikiwa imeidhinishwa au la ni vigumu mno kupata huduma za utoaji mimba kwa sababu ni ghali, mbali au kuna sheria zinazotatanisha au karatasi zinazohitaji kujazwa. Sababu hizi huwa ngumu sana haswa kwa wanawake maskini au au ambao hawaelewi huduma hizo.

Kwa bahati mbaya, katika sehemu nyingi wanawake ambao wanweza kupata huduma hiyo ni ambao wanaweza kumlipa daktari wa kibinafsi.

Utoaji mimba usioidhinishwa kisheria;- Ikiwa kuavyaa mimba hakujahalalishwa katika nchi yenu, mama anayetolewa mimba na dakatari anayefanya huduma hiyo mnaweza kukamatwa. Katika sehemu nyingi jambo hili huwa halitokei. Lakini kule ambapo hakujaidhinishwa utoaji mimba, wanawake wengi hufariki kutokana na utoaji mimba usio salama na mimba zisio salama.

MUHIMU: Usidhanie kuwa utoaji mimba si halali. Jaribu kuelewa sheria za nchi yako. Itakuwa rahisi kufanya kazi na sheria hizo kando na kuzibadilisha sheria hizo. Hata kama utoaji mimba hakujahalalishwa, kunaweza kuwa watu wanaotoa huduma zilizo salama. Kupata huduma zilizo salama kunaweza kumaanisha tofauti ya kuwa hai au kufa.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020206