Ninawezaje kutatua migogoro na mashemeji wangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ninawezaje_kutatua_migogoro_na_mashemeji_wangu

Mgogoro wowote ulionao na shemeji wako, ni muhimu sana kupata usaidizi wa mumeo ili kubadili jambo linalokusumbua. Shemeji wako ni wazazi wake, bila shaka wanampenda sana na watamsikiza mumeo sana kuliko wewe.

Kwa hiyo ni jambo zuri kupata usaidizi wake na huruma yake ili kutatua shida na shemeji wako, njia hizi zitakusaidia:-

  • Unapotafuta usaidizi kutoka kwa mumeo kuwa mtulivu, usimkemee au kulia. Muelezee mambo yanayokusumbua na uhakikishe ya kwamba ameelewa nini haswa kinachokusumbua. Ikiwa mwanzo hataelewa shida hiyo, jaribu kumueleza tena na tena hadi aelewe. Ni muhimu sana umshawishi akusaidie.
  • Jaribu sana kutomshambulia, kumwaibisha au kumuudhi. Ukifanya hivyo basi ataanza kujitetea(jambo la kawaida kwa binadamu) na hatataka kusikiza maelezo yako. Kuwa mzuri na sio mwenye hasira. Jaribu kuona kuwa yeye si shida bali yeye ni suluhisho kwa, shida inayokusumbua. Kama mume wako, yeye ni rafiki yao, sio adui. Kwa hiyo usimpe pressure bali hakikisha kuwa aelewa kwamba unahitaji msaada wake.
  • Swala moja la kawaida kwa wanandoa ni kwamba mke hutaka kutoka kwa nyumba ya wazazi wa mumeo na kutengeza familia ya nyuklia. Wakati hii inastahili kueleweka, waume wengi husita kukubaliana na swala hili. Hii ikiwa ni shida kwako, jaribu kuelewa na kuheshimu uaminifu wa mumeo kwa wazazi wake na usiwe na shauku. Badala yake jaribu kueleza kinachokusumbua kuhusu makaazi yako ya sasa, na kwa pamoja mtafute njia mbadala badala ya kumweka katika hali ya kutowaheshimu wazazi wake.

Kwa imani, mnaweza kuweka mikakati ya makao yenu badala ya kuondoka. ikiwa itawezekana mkumbushe kwa upole kwamba kama mume wako anastahili kukuheshimu pia.

  • Usifikiri ya kwamba kwa kuongea na mume wako kuhusu shauku na shida zako kutasababisha migogoro zaidi. Jambo mbaya kutokea kwa wanandoa ni kukosa kuzungumza, ikiwa hii itatendeka itaharibu hali ile, kwa hiyo mkiendelea kuzungumza itakuwa muhimu sana. Ukinyamazia shida, hisia na masikitiko yako yataongeza mawazo na wasiwasi.
  • Usifikirie kuwa mumeo hatakuelewa na shida zako na kuwa haifai kujadiliana naye. Ikiwa mwanzo hataelewa yapaswa umuelezee hadi aelewe. Wake na waume ni tofauti kwa njia kadhaa. Hufikiria, huhisi na kufanya mambo tofauti. Huishi maisha tofauti na huwa na mitazamo tofauti kwa mambo mengi. Kwa hiyo usikate tamaa ikiwa mumeo anahitaji muda kuelewa au shida unazojaribu kumueleza.

Tilia maanani mambo bora maishani mwako na kile unaweza kufanya ili uwe bora zaidi. Waweza kufanya uamuzi bora, wewe sio mnyonge.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021017