Ninawezaje kuwa na uhusiano bila ngono

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Ninawezaje_kuwa_na_uhusiano_bila_ngono

Kujenga uhusiano wa upendo unachukuwa muda, kupendana, kuheshimiana na kuaminiana kwa upande zote mbili. Ngono sio njia ya pekee ya kuonyesha unampenda mtu. Kushiriki ngono haimaanishi kuwa mtapendana.

Mnaweza kutumia muda wenu pamoja kuwa bila kushiriki ngono. Kwa kuongea na kushirikiana kuhusu maisha yenu, unaweza kujifunza mambo mengi muhimu kuhusu mwenzako - vile unavyona maisha, maamuzi mnayoweza kukubaliana kwa pamoja, vile mtakuwa kama wapenzi na wazazi, na vile mnasikia kuhusu mipango yenu binafsi kuhusu maisha. Kugusana (bila ngono) inaweza kuwaridhisha yenyewe, na haina hatari kama haitafanya mpoteze udhibiti na mshiriki ngono kabla muwe tayari.

Ongea na mpenzi wako. Ukiwa na uhakika kuwa yeye ndiye anayekufaa, lakini huna uhakika kama unataka kuwa na ngono, zungumza juu ya njia za kungoja. Unaweza pata kuwa yeye pia hayuko tayari kuwa na ngono. Kama mnaheshimiana, mtaweza kufanya maamuzi kwa pamoja.

Zungumza na marafiki. Unaweza kupata kuwa mariki wako wa kike wanapatwa pia na maamuzi haya magumu. Mnaweza saidiana kupata njia zingine za kuwa na uhusiano mzuri bila ngono. Lakini fikiria vyema kuhusu ushauri wa mwenzako ambaye ameanza kushiriki ngono. Rafiki anaweza kujaribu kukushawishi kufanya jambo amablo yeye mwenyewe anafanya ili asikie vizuri kwa kulifanya. Hii inaitwa 'shinikizo la rika'.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020812