Nitaamuwa vipi ikiwa nitatumia sheria
Maamuzi ya kutumia sheria lazima yaamuliwe vyema.
Ikiwa unafikiri ya kwamba unataka kuripoti kisa hicho kwa polisi, fanya haraka iwezekanavyo baada ya kubakwa. Usioge kabla ya kwenda, na ubebe nguo zako kwa mfuko. Vitu hivi vinaweza kuthibitisha ya kwamba ulibakwa. Nenda na rafiki yako, na mhudumu wa afya wa kike akuchunguze, ikiwa itawezekana.
Ikiwa hutaki kwenda kwa polisi, au ikiwa huwezi kwenda hadi baadaye, muone mhudumu wa afya, hata kama hujaumizwa sana. Mwambie mhudumu wa afya ya kwamba umebakwa.
Kisha atakuangalia kama uko na mikwaruzo au umeumizwa, halafu atakupa dawa ya kuzuia mimba na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Mwambie aandike chini kila kitu atakachokiona kwa sababu itasaidia kuthibitisha kwa polisi au jamii kuwa ulibakwa.