Nitachahagua vipi mbinu ya upangaji uzazi iliyo bora kwangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nitachahagua_vipi_mbinu_ya_upangaji_uzazi_iliyo_bora_kwangu

Baadhi ya maswali unayoweza kuzingatia ili kuchagua mbinu iliyo bora kwako ni:

  • Ufanisi wake wa kuzuia mimba ni upi?
  • Inazuia vipi magonjwa ya zinaa, ikiwa inazuia?
  • Ni salama kweli? Ikiwa uko na matatizo ya kiafya yallyotajwa katika sura hii, unaweza kuepuka kutumia baadhi ya mbinu za upangaji uzazi.
  • Je, ni rahisi kutumia?
  • Je, mpenzi wako angependa kutumia mbinu ya upangaji uzazi?
  • Mahitaji yako ya kibinafsi na shauku yako ni gani? Kwa mfano, uko na watoto wote unaowataka, au unamyonyesha mtoto wako?
  • Gharama ya mbinu hiyo ni ipi?
  • Je, ni rahisi kupata? Au utahitaji kutembelea kituo cha afya mara kadhaa?
  • Je, madhara (matatizo yasababishwayo) na mbinu hiyo yaweza kukuadhiri?

Baada ya kusoma kuhusu mbinu hizi, unaweza kupata msaada zaidi kwa kuchagua mojawapo. Itakuwa vyema kuzungumza na mpenzi wako, wanawake wengine, au mfanyakazi wa afya kuhusu mbinu tofauti.

Wewe pekee waweza kuamua mbinu ipi ya upangaji uzazi itakufaa.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020408