Nitaikabili vipi migogoro inayohusishwa na mahari

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nitaikabili_vipi_migogoro_inayohusishwa_na_mahari

Katika nchi nyingi kwa mfano( India, Nepal, Pakistan na Kenya)maombi, malipo au kukubaliwa kwa kiwango chochote kile kilichowasilishwa kama hitaji la kuolewa huwa imekatazwa kisheria na mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kuvunja sheria hiyo huhukumiwa chini ya sheria ya utunzaji wa watoto.

Kwa bahati mbaya, familia nyingi bado hazifahamu sheria hii na kosa lipatikanalo kwa wake na familia zao wakati mahari itashurutishwa. Wengine hufikiria kwamba kuripoti kwa polisi huenda kukawashusha hadhi. Kwa hivyo mila hii ingali ipo, haipaswi kuwa.

Mafarakano inayohusishwa na mahari bado ipo na pale wazazi wanapokosa mahari inayowaridhisha basi hukosa kumtunza vyema yule msichana na humfanya mumeo kutoa vitisho vya kumwacha yule bibi mchanga ikiwa hataleta mahari ya kutosha kutoka kwa wazazi wake.

Ikiwa unateswa na familia ya mumeo sababu ya shida ya mahari, njia hizi zinaweza kukusaidia kujitetea:-

1. Tafuta shirika la wanawake katika eneo lako(kama lipo) kupata habari na usaidizi.

2. Kama hili haliwezekani, ongea na mtu aliye na mamlaka na unayemuamini(Kwa mfano, mhudumu wa afya au kiongozi wa dini) au kwa wanwake wengine waliopitia shida kama yako. Wengine wanaweza kukupa ushauri nasaha au usaidizi kwa kuwa sio wewe pekee unayepitia shida hiyo.

3. Tafuta watu wa ukoo na majirani wanaoweza kukusaidia. Mara nyingi, kikundi cha watu wachache wanaweza kuingilia kati swala hilo na kufanya mashemeji wajue kuwa tabia yao haitakubalika.

4. Zungumza na familia yako, wazazi, ndugu zako sababu uko na haki ya kupata usaidizi kutoka kwao. Ni wajibu wao kama itahitajika kukurudisha nyumbani kwenu kukuokoa na unyanyasaji na vurugu. Kwa kuitisha msaada wao, haimaanishi kuwa wewe ni mzigo au kifaa cha msaada kwa sababu wazazi wako na jamaa yako wanafaa kupea kipao mbele maisha yako kukupa usaidizi wa kujenga tena maisha yako. Waambie ikiwa itahitajika, kama hawatataka kukuchukuwa na kukukaribisha nyumbani wataishi na hatia ya kuteswa na mauaji yako kama mashemeji wako.

5. Unaweza kuchukuwa hatua za kisheria ikiwa unaishi katika nchi ambayo mahari haikubaliwi na swala hilo huadhibiwa kisheria. Hata hivyo, unastahili kutafakari vyema kabla ya kwenda kwa polisi au kortini kwa sababu katika nchi nyingi ambapo mahari hukubalika, kwa bahati mbaya sheria zao huwa hazifanyi kazi vyema na huenda ukajichosha tu. Kwa hivyo fanya uamuzi ulio bora na kama itawezekana tafuta shirika la wanawake kabla ya kuchukuwa hatua yeyote maanake wanaweza kukusaidia kuchunguza nafasi yako ya kushinda.

Hakuna mwanamume aliye na haki ya kuweka bei kwa mkewe, au kumkubali au kumkataa kulingana na pesa au vitu atakavyoleta. Kila mwanamke anastahili kutunzwa na kuheshimiwa

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021016