Nitaitumia vipi kondomu ya wanawake Kondomu ya kike

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nitaitumia_vipi_kondomu_ya_wanawake_Kondomu_ya_kike

1. Kwa umakini fungua pakiti.

2. Utapata sehemu iliyo na umbo la pete ndani, ambayo ipo mwishoni mwa kondomu.

3. Finyilia sehemu hiyo iliyo na umbo la pete ya ndani pamoja.

4. Weka sehemu hiyo inayokaa kama pete ndani ya uke. 

5. Sukuma hiyo sehemu inayokaa kama pete juu hadi ndani ya uke wako ukitumia kidole. Sehemu inayokaa kama pete ya nje ibaki nje.

6. Wakati unapojamiiana, ongoza uume upitie kwa sehemu ya nje. 
7. Ondoa kondomu ya kike mara baada ya tendo la ngono, kabla hujasimama. Finyilia na uzungushe sehemu ya nje iliyo na umbo la pete ili kuweka shahawa ya mwanamume ndani ya pochi. Vuta pochi polepole kisha uzike mbali na watoto na wanyama. 
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020413