Nitakabiliana vipi na migogoro kuhusu upangaji uzazi na kuacha nafasi baada ya kuzaa mtoto

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nitakabiliana_vipi_na_migogoro_kuhusu_upangaji_uzazi_na_kuacha_nafasi_baada_ya_kuzaa_mtoto

Ili kutatua migogoro kuhusiana na upangaji uzazi ni muhimu uzungumze na mume wako au mpenziwe kuhusiana na njia za upangaji uzazi na njia mtakayoitumia. Ili kufanikisha mazungumzo, ni muhimu kujadili taarifa hizi na yeye:-

  • Wanawake chini ya miaka 18 ni rahisi kufariki wakati wanapojifungua kwa sababu miili yao haijakua kabisa na watoto wao wako na nafasi ya kufariki katika awamu ya kwanza ya maisha yao, kwa hiyo ni vyema kutopata watoto mapema sana.
  • Wanawake waliokomaa huwa katika hatari wanapozaa, haswa ikiwa wako na shida zingine za kiafya au walipata watoto wengi. Kwa hivyo si vizuri kuchelewa kupata watoto.
  • Mwili wa mwanamke unahitaji muda upone kati ya mimba kadhaa, kwa hivyo kuacha nafasi ya kutosha katika mimba tofauti ni salama kwa mama na watoto. Kwa hivyo ni vyema usipate watoto waliofuatana sana.
  • Mwanamke aliye na zaidi ya watoto wanne yuko na nafasi kubwa ya kufariki baada ya kuzaa kutokana na kutokwa na damu na sababu zingine. Kwa hivyo ni vyema kutopata watoto wengi sana.
  • Ukiwa na watoto wachache hautakuwa na mzigo wa kuwalea na itamsaidia mume wako kuitunza familia yake vyema. Kwa hivyo watoto wakiwa wachache familia inaweza kujikimu na kuwaelimisha vyema watoto.
  • Ukiwa na watoto wachache, wazazi watapata nafasi yao na ya watoto wao.
  • Upangaji uzazi utasaidia wanandoa kufurahia tendo la ngono kwa sababu hawaogopi kupata mimba wasizozitaka. Licha ya hayo kujikinga na mimba usioitaka haimfanyi mwanamke kutaka kujamiiana na wanaume wengine.

Ikiwa mume wako hataki mtumie njia za upangaji uzazi baada ya kujifunza umuhimu wake, ni lazima uamue ikiwa utatumia njia za kupanga uzazi ili kujikinga. Ikiwa utafanya hivyo chagua njia utakayoitumia ambayo mpenzi wako haifahamu. Haijalishi mahali ulipo, utakuwa na afya ikiwa utakuwa na udhibiti wa watoto utakaotaka na lini utakapowapata.

Kwa hivyo kuamua kutumia au kutotumia upangaji uzazi ni uamuzi wako.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021013