Nitasaidika vipi nikienda polisi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nitasaidika_vipi_nikienda_polisi

Kwa kawaida ubakaji ni uhalifu. Lakini inaweza kuchukua muda au kuwa vigumu kuthibitisha kuwa ulibakwa.

Hakikisha umesindikizwa na mtu kwa polisi.

Utaulizwa na polisi nini kilichotendeka. Ikiwa unamjua mtu aliyekubaka basi muelezee polisi. Ikiwa humjui aliyekubaka, itabidi uelezee jinsi mtu huyo anavyokaa. Polisi anaweza kuhitaji muambatane pamoja kuona kama mtampata mbakaji. Itakubidi upate ripoti kutoka kwa daktari aliyekubalika kisheria na anayefanya kazi kwa pamoja na polisi.

Ripoti hiyo ya daktari haitakusaidia kupona lakini ni dhihirisho kuwa ulibakwa. Katika nchi zingine wanawake wamefanya kazi kwa pamoja na polisi ili kuhakikisha kwamba wamepata daktari wa kike atakayehudumu kwa kuwasaidia waliyobakwa au kuhusishwa na vurugu za nyumbani.

Ikiwa mbakaji atashikwa, itabidi umtambue mbele ya jaji mahakamani au kwa polisi. Ikiwa kesi yako itasikizwa mahakamani, jaribu iwezekanavyo kumtafuta wakili ambaye ameshawahi kuwakilisha kesi za ubakaji mahakamani. Wakili huyo atakuelezea nini utakachokitarajia na atakusaidia ujiandae vyema kwa kesi yako. Hakikisha umeenda na mtu.

Kwenda kortini au mahakamani kwa kesi ya ubakaji ikiwa wewe ni muathiriwa sio rahisi. Kuelezea tena na tena kilichotokea siku uliyobakwa kunaweza kukufanya ukumbuke matukio hayo. Sio kila mtu atakuelewa, wengine wanaweza kukulaumu au kusema kuwa unadanganya.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020316