Nitatumia vipi diaphragm

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nitatumia_vipi_diaphragm

1. Ikiwa uko na spermicide, finya mpaka katikati. Kisha eneza kiasi kidogo ukitumia kidole karibu na ncha.

2. Finya diaphragm nusu nusu.

3. Fungua mdomo wa uke wako ukitumia mkono wako mwingine. Sukuma diaphragm ndani ya uke wako. Hufanya kazi ikiwa utaisukuma kuelekea upande wa nyuma wako.

4. Angalia nafasi ya diaphragm yako kwa kuweka kidole chako kimoja ndani ya uke wako na utahisi mfuko wa uzazi wako kupitia mpira wa diaphragm. Utahisi mfuko wa uzazi ni imara, kama mwisho wa pua lako. Diaphragm lazima ifunike mfuko wako wa uzazi.

5. Ikiwa diaphragm iko mahali panapostahili, hutaweza kuihisi ndani mwako.

6. Acha diaphragm katika nafasi yake kwa angalau masaa 6 baada ya kushiriki ngono.

Unaweza kuacha diaphragm ndani hadi masaa 24. Ni sawa kutumia diaphragm wakati wa siku zako za hedhi, lakini utahitajika kuiondoa na kuisafisha kama mara kadhaa kama unavyobadilisha nguo au visodo.

Kuondoa diaphragm: Weka kidole chako ndani ya uke wako. Fikisha kidole chako mwisho wa rim ya mbele ya diaphragm na uivute chini na nje. Wakati mwingine husaidia iwapo utashinikiza misuli yako kwenda chini kama vile unapojisaidia. Safisha diaphragm yako ukitumia sabuni na maji, na uikaushe. Angalia kwa kuishikilia kwa mwangaza ikiwa diaphragm iko na mashimo. Ikiwa kuna hata shimo ndogo, nunua nyingine mpya. Hifadhi diaphragm katika sehemu iliyo safi na kavu.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020415