Nitawezaje kufanya uamuzi kuhusu wavulana na ngono

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nitawezaje_kufanya_uamuzi_kuhusu_wavulana_na_ngono

Baadhi ya vijana huanza kuwa na hisia za mapenzi wanapoendelea kukua. Mawazo kuhusu kupapaswa kimapenzi ni jambo la kawaida. Mara nyingi watu huwa na hisia hizi kabla hawajakuwa tayari kufanya lolote.

Hakikisha kuwa unashiriki ngono ukiwa tayari na kama unafahamu jinsi ya kujikinga kutokana na madhara. Tendo la ngono linaeza kufurahiwa na wanaoshiriki, lakini sio kama kuna hisia za aibu au uoga.

Wasichana hushiriki ngono kwa sababu tofauti. Wengine hushiriki ngono kwa sababu wanataka mtoto. Wengine hushiriki ngono kwa sababu inawafanya wahisi wamepndwa. Kuna wengine wanaona kuwa hawana uwezo wa kuamua kwa sababu ni jukumu lao kama wake au wapenzi. Wengine hubadilisha ngono kwa pesa au kwa vitu vingine wanavyohitaji kama vile chakula, nguo za watoto au mahali pa kuishi.

Wenigne hushiriki ngono kwa sababu wanafikiria kuwa itawafanya wapendeke zaidi. Wakati mwingine rafiki au mpenzi anaweza kumshinikiza msichana ashiriki ngono, hata kama hayuko tayari.

Sio vyema kushiriki ngono ikiwa hutaki. Unaweza kushiriki ngono ikiwa uko tayari. Tendo la ngono huweza kufurahiwa na wapenzi wawili, lakini ni vigumu kufurahia kitu ambacho kinakuletea uoga na aibu, au haujakikubalia.

Ikiwa uko tayari kwa uhusiano wa kingono, hakikisha kuwa unajikinga dhidi ya magonjwa na mimba.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020809