Nitazoea vipi migogoro inayosababishwa na kuzaa mtoto wa kike

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Nitazoea_vipi_migogoro_inayosababishwa_na_kuzaa_mtoto_wa_kike

Unaweza kutumia njia zifuatazo kujitetea na kumtetea mtoto wako ikiwa mume wako au familia yake inakulazimisha kuavyaa mimba ya mtoto wa kike.

1. Muoneyeshe mume wako na familia yako kwamba bila mwanamke mtoto wa kiume hawezi kuzaliwa, kwa hivyo mtoto wa kike ni baraka katika jamii na muhimu kwa kuendeleza maisha duniani.

2. Mueleze mume wako kwamba wasichana ni nguzo muhimu katika jamii. Msichana anaweza kuwa msichana mzuri, dada mzuri, mke mzuri kisha baadaye au siku za usoni akawa mama mzuri. Ikiwa kuavyaa mimba kutaendelea kwa miaka ijayo, itafika siku ambayo hatutakuwa na akina na mama na maisha. Bila watoto wa kike hatuna maisha ya baadaye.

3. Mwambie mume wako kwamba watoto wa kike hutii sana wakilinganishwa na wa kiume. Kwa ujumla wasichana huwajibika, hujitolea na kuheshimu familia, jamii, kazi, na nchi kuliko wa kiume na huwatunza wazazi wao vyema kuliko watoto wa kiume.

4. Ikiwa mume wako na familia yake bado hawajashawishika na bado wanakulaumu kwa kupata watoto wasichana hakikisha kuwa wanaelewa mambo haya yaliyothibitishwa kisayansi(ambayo daktari au mhudumu wa afya yeyote yule atathibitisha kuwa ni ya kweli ikiwa mume wako atakuwa na shauku)

  • Jinsia ya mtoto hujulikana wakati mtu amedungwa mimba- na huwa ni shahawa ya mwanamume inayoamua ikiwa mtoto atakuwa wa kiume au wa kike. Huwa tunapata chembechembe za maumbile kutoka kwa wazazi wetu ndiposa watoto hufanana na baba na mama.
  • Kabla ya mimba kuingia, yai la mwanamke hubeba chembechembe za maumbile ziitwazo X-chromosome. Shahawa ya mwanamume hubeba X -chromosome au Y-chromosome kama chembechembe za maumbile.
  • Ikiwa shahawa iliyobeba X-chromosome itachanganyikana na yai basi kiinitete kitakuwa cha kike. Ikiwa shahawa iliyobeba X-chromosome itachanganyikana na yai kiinitete kitakuwa kijana.

Kwa hiyo shahawa ya baba huamuwa jinsia ya mtoto, sio yai la mama. Hakuna vile mwanamke anavyohusika na jinsia ya mtoto. Kwa hivyo, mumewe huhusika pakubwa na jinsia ya mtoto sio mama.

MUHIMU:Kama itawezekana usikubali kufanyiwa uchunguzi wakuonyesha jinsia ya mtoto, ikiwa mumeo au familia yake itakulazimisha kufanya uchunguzi huo tafuta usaidizi. Huenda kukawa na kikundi cha wanawake katika eneo lako ikiwa hakuna, unahitajika kuzungumza na mtu aliye na mamlaka na unaye muamini(kwa mfano mhudumu wa afya, kiongozi wa kanisa katika jamii yako au mtu aliyekomaa katika familia)

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021011