Sababu zipi nyinginezo zinazoweza kumfanya mwanamke ajiue

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Sababu_zipi_nyinginezo_zinazoweza_kumfanya_mwanamke_ajiue

Jeraha la muda: Sababu nyingine inayosababisha wanawake wengi kutaka kujiua, ni kwa sababu walipitia tukio ambalo liliwafanya wateseke na hawajui jinsi ya kukabiliana nalo. Jeraha la muda ni tukio au matukio yanayoweza kusababisha msongamano wa mawazo kimwili na /kimawazo kwa mtu na kumfanya ashindwe kukabiliana nalo na kuacha uharibifu wa kudumu.

Baadhi ya aina za kawaida zisababishazo jeraha ni pamoja na vurugu nyumbani, ubakaji, vita, mateso, na majanga ya asili. Matukio mengine yanayosababisha jeraha la kudumu kwa mwanamke ni kumpoteza mtu muhimu(kifo) au kupoteza kitu muhimu (kwa mfano: kuwapoteza wazazi, kifo cha mume au mtoto, kupoteza ajira au nyumba ), ugonjwa sugu na kuendelea kulemaa. Baadhi ya wanawake huhisi kuzidiwa na huzuni, aibu au hofu katika hali hizi, kwamba kujiua kwao ndio njia pekee ya suala hilo.

Huzuni au wasiwasi: Daima haiwachukui wanawake kupitia mambo mabaya maishani au jeraha litakalowafanya wanawake kukataa tamaa. Mara kwa mara, kiwango cha mawazo wanawake hupitia katika maisha yao ya kila siku kinaweza kusababisha unyogovu au wasiwasi, au zote mbili.

Unyogovu ni hali ya kuwa na hisia za chini au hisia ya chuki na shughuli ambayo inaweza kuathiri tabia ya mtu, mawazo, hisia na ustawi kwa kipindi cha muda mrefu. Hali ya Unyogovu, kama inavyoitwa na walio katika taaluma ya matibabu, pia husababisha ' huzuni kubwa moyoni'.

Hali ya wasiwasi kwa upande mwingine ni hisia za woga, wasiwasi na kutokuridhishwa kwa ujumla kwa kipindi cha muda mrefu. Majina mengine yanayotumika mara nyingi na hali ya wasiwasi ni: 'nerves', nervous attack' na ' mental distresses. Wakati mwanamke anapokabiliwa na dhiki nyingi kila siku na kwa muda mrefu, anaweza kuanza kuhisi kuzidiwa na kuwa hawawezi kukabiliana na majukumu yote na matatizo anayoyakabili (kwa mfano: kazi nyingi, ukosefu wa fedha/hela, ukosefu wa chakula, matatizo ya kifamilia au ya ndoa, nk).

Huzuni na wasiwasi zaweza kusababisha tabia ya kujiua, ikiwa mwanamke aliyeathirika hatapata msaada na usaidizi. Tatizo hilo linaweza kuwa baya zaidi ikiwa (kama wanawake wengi kwa ujumla)amefunzwa kuwatunza wengine kwanza na kupuuza mahitaji yake mwenyewe. Kutokana na ukosefu wa msaada wa afya ya akili katika nchi nyingi zinazoendelea, matatizo ya akili na magonjwa kama unyogovu, jeraha mara nyingi haichunguzwi au kutibiwa vilivyo, hata wakati mwanamke atakapohitaji usaidizi na msaada wa kitaalamu.

Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020907