Shida zipi za kawaida kuhusu majukumu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Shida_zipi_za_kawaida_kuhusu_majukumu

Kwa ujumla ajira ni muhimu sana kwa wanawake - wanapopata hela zao huwapa nguvu na ushawishi katika familia zao, wanazidi kujitegemea, wanakuwa watu wa hadhi ya juu katika maeneo kadhaa maishani na kuwafanya kujua watu zaidi.

Ikiwa wapendanao wanapata pesa, basi familia hiyo iko na mapato zaidi na familia hiyo yaweza kuwa na maisha bora, na wanawake wengi husema kwamba wao hujivunia na kuhisi kuridhika ikiwa wanafanya kazi na kuhusika na majukumu ya kiuchumi kwa familia zao. Ingawa, baadhi ya wanaume hawafurahishiwi pale wanawake wao wanapoweza kujitegemea na kuonyesha kujiamini.

Katika nchi nyingi na tamaduni nyingi, ni wajibu wa wanaume kutimiza mahitaji ya familia. Kwa hivyo wanawake wanapofanya kazi, wanaume wengine huogopa kupoteza nafasi zao za kitamaduni kama kichwa kwa familia na hawafurahishi pale wake wanapoachana na tamaduni za jamii yao.

Wakati mwingine wanaume huogopa kuwa wanawake wao wanaweza kuwaacha au kuwasaliti kwa kujihusisha na uhusiano na wanaume wengine wakiwa kazini mbali na nyumbani kwao. Wanaume wengine wanaamini kuwa wanawake kwa ujumla hawastahili kutoka nyumbani kwenda kazini;hufirikia kuwa wataharibika au wanawake hawana uwezo wa kufanya maamuzi dhabiti.

Wakati mwanamke anapopata hela zake, hutarajiwa kuwa na heshima, ushawishi na kutambuliwa katika familia. Kwa mfano anaweza kutaka kuhusishwa katika maamuzi ya familia hiyo (jinsi ya kutumia pesa za familia hiyo) Wanaume wengi hawafurahishwi na jambo hili na hutaka kuwa kichwa katika familia ambapo hakuna mtu anastahili kuuliza maswali mengi. Mgogoro huu wa majukumu katika familia waweza kusababisha mafarakano ya kutoelewana katika ndoa.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021005