Vipi nitakavyowalea watoto wangu vyema

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Vipi_nitakavyowalea_watoto_wangu_vyema

Ingawaje wewe na mumeo mnaweza kuwa na njia tofauti za kuwalea watoto wenu, ni vyema muweze kujadiliana na kukubaliana kwa tofauti zozote kuhakikisha kuwa mmekidhi mahitaji ya watoto wenu ambayo ni ya umuhimu kwenu.

Watoto wenu watateseka ikiwa mama yao anateseka kwa hivyo jaribu kuweka tofauti zenu kando kama itawezekana kwa ajili ya watoto wenu.

Kama itahitajika mkumbushe mumeo ya kuwa uhusiano unaopendeza kati ya wazazi ni bora kisaikolojia na kwa ustawi wa mahitaji ya kimwili ya watoto wao na ukumbuke ya kwamba kama wamama kila siku tunawafunza watoto wetu kwamba:-

  • Njaa ya wanawake na wasichana haijalishi sana tukiwalisha waume na vijana wetu kwanza.
  • Wasichana hawahitaji nafasi itokanayo na elimu tunapowapeleka vijana wetu shuleni.
  • Tunakuza vijana kuwa na vurugu ikiwa tutawafunza kuwa mwanamume lazima awe na vurugu.
  • Tunawafunza vijana wetu kuwa inakubalika kwa mwanamume kumchapa mkewe na watoto ikiwa hatutazungumzia vurugu inayoshuhudiwa kwa jirani.

Kama wanawake tunauwezo wa kubadilisha jinsi watoto wetu watakavyokuwa, na tunaweza kuwafunza:-

  • Vijana wetu kuwa na utu na huruma, ndiposa wawe waume, ndugu na baba waliojaa utu na huruma.
  • Wasichana wetu kujidhamini ndiposa wadhaminiwe na wengine.
  • Vijana wetu kusaidia katika shughuli za nyumbani ndiposa dada, wake na watoto wao wasilemewe na kazi za nyumbani.
  • Wasichana kujitegemea sana kwa kumaliza shule au kujifunza ujuzi fulani.
  • Vijana kuwaheshimu wanawake wote na kuwa wapenzi walioajibika.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021018