Wakati upi nitakapo ACHA kutumia kidonge na nimuone mhudumu wa afya

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Wakati_upi_nitakapo_ACHA_kutumia_kidonge_na_nimuone_mhudumu_wa_afya

ACHA kutumia kidonge na umuone mhudumu wa afya ikiwa:
* utakuwa na maumivu makali ya kichwa na Kiwaa ( migraines ) kinachoanza baada ya kumeza kidonge. 
  • utahisi udhaifu au kufa ganzi katika mikono au miguu yako.
  • utahisi maumivu makali katika kifua chako na kushuhudia upungufu wa kupumua.
  • utakuwa na maumivu makali katika mguu mmoja.
  • utakuwa na maumivu makali ya tumbo.

Ikiwa uko na matatizo haya, mimba inaweza pia kuwa hatari, hivyo basi tumia mbinu nyingine ya upangaji uzazi kama vile kondomu hadi pale utakapomuona mhudumu wa afya aliye na ujuzi wa masuala ya mbinu za homoni za upangaji uzazi.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020425