Wanawake huadhirika kivipi kutokana na vurugu ya wanaume

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Wanawake_huadhirika_kivipi_kutokana_na_vurugu_ya_wanaume

Kwa wanawake, vurugu inayosababishwa na wanaume yaweza kusababisha:

  • Ukosefu wa motisha au ukosefu wa hisia ya kujithamini.
  • Matatizo ya afya ya akili, kama wasiwasi na matatizo ya kula na kulala. Kama njia ya kukabiliana na vurugu, wanawake wanaweza kuanza tabia zinazowadhuru - kama vile kutumia madawa ya kulevya au pombe, au kuwa na wapenzi wengi.
  • Maumivu makali na majeraha: kuvunjika kwa mifupa, kuchomeka, macho meusi, pamoja na, kuumwa kichwa, maumivu ya tumbo, na maumivu ya misuli ambayo yanaweza kuendelea kwa miaka mingi baada ya unyanyasaji kutokea.
  • Matatizo ya afya ya kujamiiana. Wanawake wengi mimba hutoka kwa sababu ya kuchapwa wakati wa ujauzito. Wanaweza pia kukabiliwa na mimba wasizozihitaji, magonjwa ya zinaa (STIs) au kuambukizwa VVU kama matokeo ya unyanyasaji wa kijinsia.

Unyanyasaji wa kijinsia mara nyingi husababisha hofu ya kujamiiana, maumivu wakati wa kujamiiana, na ukosefu wa hamu.

  • Kifo.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020111