Wanawake wagani wanapaswa kuepuka aina yoyote ile ya mbinu ya homoni

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search
QR for this page

https://www.audiopedia.org/Wanawake_wagani_wanapaswa_kuepuka_aina_yoyote_ile_ya_mbinu_ya_homoni

Wanawake walio na saratani ya matiti, au donge ngumu katika matiti. Mbinu za homoni hazisababishi saratani. Lakini ikiwa mwanamke tayari yuko na saratani ya matiti, mbinu hizi zinaweza kuharibu mambo.

Wanawake ambao wanaweza kuwa na mimba au ambao huchelewa kupata hedhi.

Wanawake wanao tokwa na damu isiyokuwa ya kawaida ukeni wakati wa miezi 3 kabla ya kutumia mbinu za homoni. Wanastahili kumuona mhudumu wa afya ili kutambua ikiwa kuna tatizo kubwa.

Baadhi ya mbinu za homoni ni hatari kwa wanawake walio na matatizo mengine ya afya. Hakikisha umeangalia mbinu zote ili kuona ikiwa ni salama kwa matumizi yako. Ikiwa uko na matatizo yoyote ya afya yaliyotajwa na bado unataka kutumia mbinu, zungumza na mhudumu wa afya aliye na ujuzi wa mbinu za homoni za upangaji uzazi.

Madawa mengine ya kifafa yajulikanayo kama ( "fits"), ya kifua kikuu (TB), au ya VVU hufanya mbinu za homoni kutofanya kazi vyema. Mwanamke anayetumia dawa hizi lazima atumie mbinu zingine au achanganye na mbinu ya pili kama kondomu au diaphragm.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020419